Baada ya kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Yanga imejihakikishia kuvuna kitita cha zaidi ya Tsh Bil 1.9 (dola 700,000)
Jumla mpaka sasa Yanga itakuwa imevuna zaidi ya Tsh Bil 2.2 fedha za bonas ya CAF kuanzia hatua ya awali na Tsh Milioni 85 za goli la Mama
Yanga itavuna 'mkwanja' zaidi wa CAF kama itasonga mbele na kufika mbali zaidi katika michuano hiyo
Kama Yanga itatinga robo fainali itavuna takribani Bil 2.5, nusu fainali dau litaongezeka na kufika Bil 3.3
Fainali dau ni Bil 5.4 wakati kama Yanga itafanikiwa kutwaa ubingwa itavuna takribani Bil 10.9
ADVERTISE HERE