Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki ana jambo lake katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu
Aziz Ki aliyekuwa MVP na mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC msimu uliopita, amemaliza kinara wa mabao katika hatua ya awali ya ligi ya mabingwa
Aziz Ki amefunga hesabu za hatua ya awali akiwa na mabao matano sawa na Youcef Belail wa Esperance ya Tunisia
Aidha Prince Dube, Clatous Chama na Clement Mzize nao wanafuatia kwa karibu kila mmoja akiwa amepachika mabao matatu
Kama alivyomaliza msimu uliopia, Ki amerejea msimu huu akiwa na kiu zaidi na wananchi watarajie makubwa zaidi kutoka kwake kuanzia hatua ya makundi ya CAF CL na huku kwenye ligi na michuano mingine
ADVERTISE HERE