Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema ataendelea kumtumia winga Denis Nkane katika majukumu ya ulinzi upande wa kulia kwani amejiridhisha anamudu kucheza katika eneo hilo kulingana na mbinu zake
Katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya CBE SA uliopigwa Zanzibar na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 6-0, Gamondi alimuingiza Nkane katika kipindi cha pili akichukua nafasi ya Yao Kouassi
Gamondi amesema kwa mbinu ambazo hupendelea kutumia, majukumu ya mlinzi wa kulia wakati mwingine ni kama winga, hivyo haoni tatizo kumtumia Nkane katika eneo hilo
Lakini pia amesema kutokana na ushindani uliopo, sio rahisi kwa Nkane kupata nafasi mbele ya wachezaji kama Maxi Nzengeli, Clement Mzize, Clatous Chama, Kennedy Musonda na Pacome Zouzoua ambao hutumika kama mawinga katika nyakati toafuti
"Denis Nkane kwangu namuona ana uwezo wa kuwa beki wa pembeni anayeweza kushambulia (wingback) kwasababu ana kasi na ujuzi, naamini hii nafasi itamjenga kuwa bora zaidi kwenye siku za usoni," alisema Gamondi