Kiungo wa Yanga, Aziz Andabwile amesema wanafahamu kilichowahi kuwakuta mkoani Mbeya, Yanga alipopoteza mechi zake dhidi ya Ihefu kwa misimu miwili mfululizo, hivyo watakuwa makini na tahadhari kubwa kufikia malengo.
Kwenye michezo miwili ya ugenini mkoani Mbeya, Yanga ilifungwa mabao 2-1 msimu wa 2022/23 na 2023/23 na imekuwa ni mechi ngumu kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ikiwa mkoani humo.
Yanga inashuka uwanjani leo kuanzia saa 10:15 jioni kuivaa Gen Gold ikiwa ni mchezo wake wa pili baada ya kumaliza michezo ya kimataifa na kufuzu makundi na Kocha Miguel Gamondi alisema anachokitaka ni pointi tatu na kama wapinzani wao wakijichanganya watatumia vilivyo nafasi kwenye mechi hiyo Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
KenGold ambayo hivi karibuni iliachana na kocha wake mkuu, Fikiri Elias na msaidizi wake Luhaga Makunja, haijashinda wala kupata sare tangu msimu uanze.
Yanga imeshuka dimbani mara saba kwenye michuano yote na kushinda mechi zote. Imepachika mabao 24 na kuruhusu moja pekee. KenGold, mechi nne za ligi ilizocheza msimu huu imepoteza zote ikifunga mabao mawili na kuruhusu nane. Inashika nafasi ya mwisho katika msimamo