Katika mechi tatu ambazo Yanga imecheza kwenye ligi mpaka sasa msimu huu, hakuna mwamuzi aliyelalamikiwa baada ya dakika 90
Maana yake ni kuwa Yanga imeshinda mechi zake tatu kwa uwazi pasipo kuhitaji makosa ya kibinadamu ya waamuzi, hili ni jambo muhimu
Mashabiki wa Yanga hawapaswi kuwa na presha yoyote kwani timu yao inashinda kihalali katika msimu ambao timu nyingi zimejipanga
Kuna timu zimelazimika kutegemea makosa ya kibinadamu ya waamuzi kushangilia ushindi pengine kama waamuzi wasingefanya makosa hayo matokeo yangekuwa tofauti
Hata siku moja timu inayopambana uwanjani kupata matokeo halali haiwezi kushindanishwa na timu zinazotegemea zaidi waamuzi
Na hapa ndipo Wananchi wanapaswa kujikita, kupiga kelele ili TFF na Bodi ya ligi wachukue hatua kwa waamuzi ambao wanaonekana kuzinufaisha baadhi ya timu
Timu moja haiwezi kunufaika na makosa ya waamuzi katika mechi mfululizo halafu jambo hili likaonekana ni bahati mbaya
Kabla ya msimu kuanza, TFF waliwahakikishia wadau wa soka Tanzania kuwa msimu huu VAR itatumika lakini imekuwa kinyume
Ni wakati wa kuhoji imekuwaje VAR haitumiki na katika kipindi hiki makosa ya kibinadamu yanazidi kuongezeka hasa katika mechi za Simba? Kulikoni?
Bodi ya Ligi na Kamati ya waamuzi wanachukua hatua gani kukomesha hili? Tunajua waamuzi ni binadamu, wanakosea lakini kuna makosa wanafanya yanaibua maswali