Yanga iko mkoani Morogoro ikiendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Simba utakaopigwa Jumapili ijayo, April 29 2018.
Baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Mbeya City Yanga ilirejea Morogoro, mahali ambapo imekuwa ikiweka kambi siku zote.
Simba nayo imeweka kambi mkoani humo.
Tayari wachezaji waliokuwa wameachwa jijini Dar es salaam wameungana na wenzao.
Ibrahim Ajib na Andrew Vicent hawakusafiri na kikosi cha Yanga mkoani Mbeya, wameungana wenzao mapema jana.
Naye Amissi Tambwe amejumuika na wachezaji wa yanga mkoani humo kujiandaa na mchezo huo.
Yanga inahitaji kuibuka na ushindi dhidi ya Simba ili kurejesha matumaini ya kutetea ubingwa msimu huu.

ADVERTISE HERE