Baada ya Yanga kupata mafanikio makubwa katika misimu mitatu iliyopita, ni wazi msimu huu lazima kuwa imara zaidi ili kuendelea kubaki juu
Kuna vita kubwa inapaswa kupiganwa ndani ya uwanja na huko nje ya uwanja ili kuhakikisha timu haitoki kwenye reli
Hata haya matokeo ya 1-0 ambayo yanaonekana kuwakera Wananchi pengine ni matokeo ya athari za yale yanayoendelea 'nje'
Hapa tunawakumbusha Wazee wa Yanga, kina Mzee Mpili na wenzake hawapaswi kulala kwani kuna kila dalili mashambulizi kutoka nje yameanza kuathiri ufanisi wa wachezaji wa Yanga, hili sio jambo la kupuuza! Mpira wa Afrika sote tunaujua!
Katika mechi za karibuni wachezaji wa Yanga wamekosa nafasi nyingi sana katika mazingira ya kushangaza
Angalia mechi ya kwanza ya ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar, mechi ya ligi ya mabingwa dhidi ya CBE SA kule Ethiopia, angalia mechi dhidi ya Ken Gold na mechi dhidi ya KMC juzi
Hizi ni mechi ambazo Yanga ingefunga zaidi ya mabao matano katika kila mechi kama nafasi zingetumika kwa usahihi wake
Haya mambo sio ya kupuuza kwani yalishawahi kuiumiza Yanga misimu michache nyuma
Msimu wa 2021/22 Fiston Mayele wakati yuko Yanga alianza msimu na kasi kubwa ya kuzifumania nyavu. Lakini ghafla umahiri wake ukapotea mpaka pale Wazee walipoingilia kati kuondoa 'kiwingu'Β
Hivyo, wakati kocha Miguel Gamondi akifanyia kazi changamoto zinazoonekana katika kiwanja cha mazoezi, basi wazee nao hebu waingie 'mzigoni' kutegua mitego yote ambayo yawezekana kabisa imetegwa