Bao alilofunga katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji jana, linamfanya Maxi Nzengeli awe kinara wa mabao katika kikosi cha Yanga msimu huu akiwa na mabao matatu
Katika mechi ambazo Yanga wamecheza mpaka sasa, Maxi amefunga kwenye mechi tatu dhidi ya Kagera Sugar, KMC na Pamba Jiji
Jana Maxi pia aliandikisha 'assist' yake ya kwanza msimu huu akiwa sawa na Pacome Zouzoua mwenye assist moja pia
Kinara wa kutoa pasi za mabao ni Stephane Aziz Ki mwenye assist mbili akiwa amepachika bao 1 pia
IBrahim Bacca ndiye anayefuatia katika orodha ya wafungaji wa Yanga akiwa na mabao mawili
Bacca ameweka ahadi msimu huu anataka kuwania tuzo ya ufungaji bora. Tayari ameweka rekodi mpya kwani tangu alipotua Yanga hakuwa amefunga bao lakini sasa anayo mawili
Clement Mzize na Kennedy Musonda ndio wanakamilisha idadi ya mabao nane ambayo Yanga wamefunga msimu huu pasipo kuruhusu nyavu zao kutikiswa