Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imeanza mazoezi kujiandaa na michezo miwili ya kufuzu AFCON 2025 dhidi ya DR Congo itakayochezwa Oktoba 10 na Oktoba 15, 2024Β
Mechi ya kwanza itapigwa DR Congo na mchezo wa marudiano kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
DR Congo ndio vinara wa kundi H wakishinda mechi zao mbili na kukusanya alama sita huku Tanzania ikifuatia nafasi ya pili ikishinda mechi moja na kutoka sare mechi moja
Ni wazi mechi hizi dhidi ya DR Congo zinaweza kutoa mwanga juu ya hatma ya Tanzania kushiriki fainali za Afcon 2025 zitakazofanyika Morocco
ADVERTISE HERE