Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema hana wasiwasi wowote kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba ambao utapigwa baada ya mapumziko ya kalenda ya CAF
Watani wa jadi Simba na Yanga watachuana katika mchezo wa kwanza ligi kuu msimu huu utakaopigwa Oktoba 19 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Gamondi amesema kwake mchezo huo hauna tofauti na mechi nyingine za ligi hivyo maandalizi yake hayatakuwa na utofauti
"Kwangu mimi kuniuliza leo kuhusu mechi dhidi ya Simba sioni sababu maana kuna wiki mbili zaidi"
"Lakini pia ni mechi kubwa kwa mashabiki lakini kwangu naona ni mechi kama mechi zingine tu na maandalizi ni yale yale kama dhidi ya timu nyingine utofauti ni kuwa inachezwa uwanja wa Benjamin Mkapa," alisema Gamondi
Tangu alipojiunga na Yanga msimu uliopita, Gamondi ameweka rekodi ya aina yake akishinda mechi tatu dhidi ya Simba kikosi chake kikifunga jumla ya mabao 8-1
Kipigo kizito zaidi ilikuwa 5-1 ukiwa mchezo wa raundi ya kwanza ligi kuu msimu uliopita