Yanga imepata dawa ya 'mipira iliyokufa'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Oct 2024
Yanga imepata dawa ya 'mipira iliyokufa'

Pamoja na ubora, katika misimu ya karibuni Yanga imekosolewa zaidi kwa kushindwa kutumia vyema mipira ya adhabu

Ukiacha mapigo ya moja kwa moja ambayo mara kadha Stephane Aziz Ki amefunga na hata Clatous Chama, ni nadra sana Yanga kufunga kupitia mipira ya kona na mapigo mengine ya adhabu ambayo sio moja kwa moja

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amefichua kuwa kazi kubwa imefanyika katika kiwanja cha mazoezi na hivyo msimu huu Yanga imejipanga kufunga mabao mengi kupitia mipira hiyo

Kudhihirisha hilo tayari beki Ibrahim Bacca amefunga mabao mawili akimalizia mapigo ya mipira ya kutenga

Gamondi amesema amegundua katika Ligi Kuu Tanzania Bara, mipira ya faulo inapatikana mingi, lakini imekuwa haitumiwi vizuri, hivyo ametengeneza mafunzo maalum kwa nyota wake ili waweze kupata mabao kwa njia hiyo

"Kwa sasa tumejifunza jinsi ya kupata mabao kwa njia ya faulo, kila kitu tumekifanyia mazoezi, katika ligi ya Tanzania wachezaji wanafanya faulo nyingi sana, kama zinatumiwa vizuri, tunaweza kupata mabao mengi na ndivyo ninavyofanya sasa," alisema Gamondi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’