Bodi ya ligi yathibitisha kupokea malalamiko ya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Apr 2018
Bodi ya ligi yathibitisha kupokea malalamiko ya Yanga
Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi kuu ya Vodacom Boniface Wambura amethibitisha Bodi hiyo kupokea malalamiko Yanga dhidi ya klabu ya Mbeya City.

Wambura amesema rufaa ya Yanga imewasilishwa kwa Kamati ya Saa 72 ambayo inasubiri ripoti ya mwamuzi na kamishna wa mchezo huo.

Ò€œTumepata malalamiko ya Yanga kwa hiyo tunapeleka kwenye kamati inayohusika kwa ajili ya maamuzi na kikanuni tunasubiri ripoti ya mwamuzi na kamishna ambazo tunatakiwa tuzipate ndani ya saa 48Ò€ amesema Wambura

Kimsingi Yanga imewasilisha malalamiko matatu kwa Bodi hiyo ya ligi.

1. Vurugu zilizofanywa na mashabiki wa Mbeya City kwenye dakika ya 66 kupelekea mchezo huo kusimama kwa dakika kadhaa wakati jeshi la Polisi likituliza vurugu hizo.

Wakati mchezo ukiendelea mashabiki wa Mbeya City walikuwa wakimrushia mawe mlinda lango wa Yanga Youthe Rostand ambaye mara kadhaa alilazimika kulikimbia lango kunusuru maisha yake.

Kwa kiasi kikubwa hali hiyo ilisababisha taharuki kwa wachezaji wa Yanga hivyo kuwaondoa mchezoni.

2. Tukio la Malima aliyetolewa nje kwa kadi nyekundu kurejea uwanjani kushangilia na wenzie baada ya Mbeya City kusawazisha bao kwenye dakika ya 90.

3. Kitendo cha Mbeya City kuzidisha idadi ya wachezaji waliostahili kuwepo uwanjani.

Kwenye dakika za nyongeza kuna mchezaji aliumia akatolewa nje kwa ajili ya kupatiwa huduma ya kwanza.

Wakati akiwa nje benchi la ufundi la Mbeya City lilimfanyia mabadiliko lakini baada ya kutibiwa akarudi tena uwanjani na kuendelea kucheza na hivyo kufanya idadi ya wachezaji wa Mbeya City kuwa 11 wakati tayari mchezaji mmoja alikuwa ametolewa nje kwa kdai nyekundu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’