Bacca amepania kufunga Kariakoo dabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Oct 2024
Bacca amepania kufunga Kariakoo dabi

Beki wa Kati wa Yanga, Ibrahim Hamad 'Bacca', amesema katika mwendelezo wake wa kusaka kiatu cha dhahabu, anatamani pia kufunga bao katika mechi ijayo dhidi ya Simba, itakayopigwa Oktoba 19, mwaka huu

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Bacca alisema kwa sasa anatamani kufunga bao kwenye kila mchezo ambao timu yake inacheza hasa kwenye Ligi Kuu ambako ameamua kuingia rasmi kwenye kinyang'anyiro cha kuwania ufungaji bora

Bacca, aliwashangaza mashabiki wa soka baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya KenGold, Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, akisema kuwa ameingia rasmi kwenye kinyang'anyiro cha kuwania ufungaji bora msimu huu

Ilikuwa ni baada ya kufunga bao pekee kwenye mchezo huo uliopigwa uwanjani hapo Septemba 26, mwaka huu, Yanga ikishinda bao 1-0. Ilionekana kama ni kufurahisha baraza, lakini waliwashtua wengi alipopachika tena bao, Alhamisi iliyopita, Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, Yanga iliposhinda mabao 4-0, dhidi ya Pamba Jiji FC

"Wale waliokuwa wanadhani mimi natania nadhani wameanza kuamini, kama nilivyoweka ahadi yangu, nadhani huu ni mwanzo tu, unajua baada ya kufunga bao moja kule Mbeya, akili yangu sasa nataka kufunga bao kila mchezo unaokuja, na utakaofuata unajua tunacheza na nani Oktoba 19, nataka pia kufunga bao," alisema beki huyo ambaye pia anaichezea timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars

Bacca ambaye kwa sasa yupo kambini na Stars, alisema angekuwa na mabao matatu kama si kukatazwa kwenda kupiga penalti katika mchezo dhidi ya Pamba Jiji

"Unaona hata ile penalti ilipotokea nilitaka kupiga mimi mwenyewe kuendeleza nilichoahidi, saa hizi ningekuwa na mabao matatu, anayeongoza kwenye ufungaji mpaka sasa si ana mabao matano jamani? Sasa matatu si yangebaki mawili tu, tungekuwa tunafukuzana," alisema Bacca na kulalamika juu ya kukatazwa kupiga penalti na nahodha wake, Bakari Mwamnyeto

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’