Hawa Al Hilal tuna kazi nao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Oct 2024
Hawa Al Hilal tuna kazi nao

Droo ya hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ilifanyika Misri juzi Yanga ikipangwa kundi A pamoja na timu za TP Mazembe, Al Hilal na MC Alger

Mechi ya kwanza ya makundi itapigwa Novemba 26/27 Yanga ikianzia nyumbani dhidi ya Al Hilal

Hii itakuwa mechi ya kisasi kwa Yanga kwani Wananchi wanakumbuka kilichotokea misimu miwili iliyopita katika hatua ya awali pale palipokutana na Al Hilal katika ligi ya mabingwa

Mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 na mechi ya marudiano iliyopigwa Sudan wiki moja baadae, Al Hilal wakapata ushindi wa bao 1-0 na hivyo kutinga hatua ya makundi huku Yanga ikidondokea katika kombe la Shirikisho ambako walifanikiwa kuwaondoa Club Africain na moja kwa moja kucheza makundi katika msimu ambao Yanga ilicheza fainali CAF CC

Ni kumbukumbu hii ambayo inapelekea mechi mbili dhidi ya Al Hilal katika makundi kuwa umuhimu wa kipekee kwa Yanga

Yanga inazihitaji alama zote sita dhidi ya Al Hilal ambao mechi zao za nyumbani watachezea Libya

Wananchi wanasema Al Hilal wameingia kwenye mfumo, ni wakati wa kupipa kisasi..!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16m ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’