Tanzania imeshindwa kutamba ugenini ikikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya DR Congo katika mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2025 kundi H
Bao pekee la DR Congo lilipatikana katika dakika ya 54 baada ya mpira wa kona kumgonga Clement Mzize na kujaa kimiani
Stars ilikuwa na nidhamu nzuri katika ulinzi lakini hawakutengeneza nafasi nyingi langoni kwa DR Congo
Kocha Hemed Morocco na vijana wake wana siku tano za kujiuliza kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Oktoba 15
Stars inahitaji kushinda mchezo huo ili kuweka hai matumaini ya kushiriki Afcon 2025 itakayofanyika Morocco
ADVERTISE HERE