Kiungo mshamuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki jana aliiongoza Burkina Faso kupata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Burundi katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afcon 2025
Aziz Ki alikuwa sehemu ya kikosi kilichoanza mchezo huo akicheza kwa takribani dakika 70
Ni ushindi ambao umeipeleka Burkina Faso kileleni mwa kundi L baada ya kufikisha alama 7
Nyota wengine wa Yanga waliokuwa uwanjani katika majukumu ya timu za Taifa jana ni pamoja na Prince Dube ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Zimbabwe kilichopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namibia akiingia kipindi cha pili
Ibrahim Bacca, Dickson Job, Mudathir Yahya na Clement Mzize wao walikuwa sehemu ya kikosi cha Tanzania kilichopoteza mchezo dhidi ya DR Congo kwa kufungwa bao 1-0
Leo Clatous Chama, Kennedy Musonda (Zambia), Khalid Aucho (Uganda) na Duke Abuya (Kenya) nao wanatarajiwa kushuka dimbani kuzitumikia timu zao za Taifa