Mshambuliaji wa Yanga Kennedy Musonda leo amefunga bao pekee la ushindi kwa timu yake ya Taifa ya Zambia katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afcon 2025 dhidi ya Chad
Ni ushindi ambao umeipandisha Zambia katika nafasi ya pili kundi G baada ya kufikisha alama 7 alama mbili nyuma ya Ivory Coast yenye alama 9
Nayo Uganda ikiongozwa na nahodha Khalid Aucho, inakaribia kujihakikishia tiketi ya kufuzu Afcon 2025 baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sudan Kusini
Kama Afrika Kusini itapata ushindi dhidi ya Congo, mbio za kundi K zitahitimishwa kwa Uganda na Afrika Kusini kufuzu
Mlinda lango Djigui Diarra atakamilisha majukumu ya timu ya Taifa baade pale Mali itakapokuwa ugenini kuikabili Guinea Bissau katika mchezo ambao kama Mali itashinda basi itafuzu Afcon 2025