Kabla ya mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba dhidi ya Yanga uliopigwa jana uwanja wa Benjamin Mkapa na Wananchi kuibuka na ushindi wa bao 1-0, mshambuliaji wa Simba Lionel Ateba alitamba kuwa hawahofii mabeki wa Yanga na kuwa lazima angefunga katika mchezo huo
Ateba alikwenda mbali zaidi na tambo zake baada ya 'Koplo' Ibrahim Bacca kutoa taarifa ya majeraha aliyopata wakati akiitumikia timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' akidai anaogopwa ndio maana visingizio vya majeruhi
Hata hivyo baada ya dakika 90 za mchezo wa jana, Ateba atakuwa amefahamu daraja la mabeki wa Yanga
Ukiacha nafasi aliyopata dakika za mwanzo ambapo mlinda lango Djigui Diarra alifanya kazi yake vyema, Ateba hakuliona lango la Yanga
Mshambuliaji huyo raia wa Cameroon hakuweza kupiga shuti lolote liwe limelenga lango au kutoka nje
Bacca amemkunbusha Ateba kuwa anapaswa kuheshimu mpira wa miguu na zaidi anapaswa kuheshimu mpinzani anayekutana nae