Kama sio ujasiri wa kocha Miguel Gamondi pengine mlinda lango Djigui Diarra asingeanza jana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0
Diarra alichelewa kurejea nchini kutoka Guinea Bissau alikoitumikia timu ya Taifa ya Mali ambapo mlinda lango huyo alitua Tanzania jana saa chache kabla ya mchezo
Tayari maamuzi yalikuwa yameshafanyika kutomtumia katika mchezo huo lakini baada ya yeye mwenyewe kumuhakikishia Gamondi na benchi la ufundi kuwa yuko tayari kucheza, moja kwa moja akaingia kikosini
Kuchelewa kwa Diarra kulitengeneza presha, inafahamika mchezo wa dabi siku zote inapotokea mazingira ya sintofahamu kwa mchezaji lazima kuwe na mashaka
Gamondi aliamini sababu zilizotolewa na mchezaji wake kupelekea kuchelewa kurudi na kuthibitisha hakukuwa na changamoto yoyote nje ya uwanja akampanga licha ya kutua nchini takribani saa tatu kabla ya mchezo
Ndani ya dakika 5 za mchezo huo Diarra akafanya 'save' mbili muhimu ambazo ziliiweka Yanga mchezoni na akahakikisha anaondoka na 'cleansheet' ya tano msimu huu
Jana Diarra amedhihirisha yuko tayari kuipigania Yanga wakati wowote na haishangazi kwa nyota huyo kusaini mkataba wa miaka mitatu mwanzoni mwa msimu licha ya kuwa na ofa nyingi kutoka nje