Msimu uliopita Yanga iliweka rekodi ya aina yake kwa kushinda mechi zote 15 ilizocheza nyumbani katika ligi kuu ya NBC
Msimu huu tayari Yanga imeshinda mechi tatu katika uwanja wa nyumbani na kuendeleza rekodi hiyo
Lakini kubwa zaidi ni kuwa takwimu zinaonyesha Yanga sasa imecheza takribani mechi 50 nyumbani pasipo kupoteza
Yaani Wananchi ni 'unbeaten' kwa mechi 50 nyumbani, wakishinda mechi 45 na kutoka sare mechi 5
Msimu wa 2022/23 Wananchi waliweka rekodi ya kucheza mechi 49 bila kupoteza (nyumbani na ugenini), sasa wameweka rekodi nyingine kama hiyo kwa mechi za nyumbani
Kwa hakika Yanga iko katika nyakati bora sana, katika kipindi hiki yasiyowezekana yamewezekana!
ADVERTISE HERE