Yanga kamili kuikabili Coastal Union huko Arusha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Oct 2024
Yanga kamili kuikabili Coastal Union huko Arusha

Kikosi cha Yanga tayari kiko mkoani Arusha kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union utakaopigwa kesho Jumamosi, Oktoba 26 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Msafara wa Yanga ulitua Arusha jana usiku ambapo vijana wa Kocha Miguel Gamondi leo watakamilisha maandalizi yao ya mwisho katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid

Akizungumza kuelekea mchezo huo, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki na wanachama wa Yanga kujitokeza kwa wingi dimba la Shekh Amri Abeid kuishangilia timu yao hapo kesho

Licha ya ugumu wa ratiba ambapo Yanga inashuka dimbani kwa wastani wa kila baada ya siku tatu, Kamwe amesema kocha Gamondi ataendelea na utaratibu wa kufanya 'rotation' ili kulinda afya za wachezaji

Nae beki Ibrahim Bacca amesema mara nyingi mechi zinazopigwa mikoani zinakuwa ngumu lakini wachezaji wamejipanga ili kuhakikisha wanawapa furaha mashabiki wao kwa kushinda mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kamwe apongeza TFF kupima dawa za kusisimua miili
Kamwe apongeza TFF kupima dawa za kusisimua miili
1h ago
READ MORE β†’
Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
Yanga imepania kuiwekea rekodi CFFA
6h ago
READ MORE β†’
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
Ngoma wakati utafika, atapewa heshima yake
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 20, 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mwenda aanza mazoezi Yanga
Mwenda aanza mazoezi Yanga
22h ago
READ MORE β†’
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
Viingilio; Yanga vs CFFA, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
Jumatano tuweke rekodi pamoja - Kamwe
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
Yanga yaweka rekodi ya mabao raundi ya pili CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
TFF kuwabaini wanaotumia dawa za kusisimua misuli Ligi Kuu
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 19 2026
1d ago
READ MORE β†’