Baada ya ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha jana, kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es salaam kukamilisha maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Singida BS
Ni mwendo wa bandika bandua kwa Wananchi kwani wana siku mbili tu za kujiandaa kabla ya kuelekea Zanzibar kuikabili Singida BS, Jumatano Oktoba 30 katika uwanja wa New Amaan Complex
Baada ya mchezo huo Yanga itarejea jijini Dar es salaam kuikabili Azam Fc, Jumamosi Novemba 02 2024
Ushindi katika mechi hizi mbili zinazofuata, utaiweka Yanga katika nafasi nzuri katika malengo ya kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo
ADVERTISE HERE