Mlinzi wa kulia wa Yanga Kibwana Shomari amerud Gym kuimarisha 'fitness' yake ili kuhakikisha anarejea katika kikosi cha kwanza
Kibwana amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kocha Miguel Gamondi sababu kuu ikitajwa makali yake kupungua
Mara kadhaa Gamondi amelazimika kuwatumia Maxi Nzengeli, Denis Nkane na hata Dickson Job katika baadhi ya nyakati anapokosekana Yao Kouassi
Hata hivyo, katika mahojiano aliyofanya hivi karibuni, Gamondi hakutaka kuzungumza kwa kina sababu ya kutomtumia Kibwana lakini akasisitiza hakuna tatizo
"Ni maamuzi yangu nina wachezaji wengi kwenye nafasi tofauti, kama timu inafanya vizuri kwanini nifanye mabadiliko kwa wachezaji na hili ni jukumu langu"
"Nina mazungumzo mazuri sana na wachezaji na kuna wachezaji wengi pia hawachezi na wapo vizuri," alisema
Gamondi ameweka msimamo kwa wachezaji wake kuhakikisha wanakuwa katika ubora muda wote ili kuwa na nafasi ya kucheza