Klabu ya Yanga leo imesaini Mkataba wa huduma za afya na elimu kwa UMMA na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)Β
Pamoja na kutoa elimu kwa UMMA kuhusu magonjwa ya moyo, Mkataba huo pia utawanufaisha Wanachama na Mashabiki wa Yanga kwa kupata punguzo pale wanakwenda kutibiwa katika Taasisi ya JKCI
Afisa Mtendaji Mkuu wa Yanga Andre Mtine amesema Yanga imepewa heshima kubwa kushirikiana na JKCI katika kuelimisha UMMA kuhusu magonjwa ya moyo
"Kila mtu anajua taifa lenye watu wenye afya nzuri ndio taifa lenye furaha zaidi. Kila mtu anafahamu afya ndio chachu ya maendeleo kwa taifa lolote. Kwa kutambua hilo Klabu ya Yanga imejitanabaisha kwa kuingia Ubia na Taasisi hii ya Moyo katika kutoa elimu kuhusu magonjwa ya moyo"
"Ni heshima kubwa sana kwetu (Yanga) kupata fursa hii ya kujumuika na Taasisi hii ya Moyo katika safari yao ya kutoa elimu chanya kuhusu magonjwa ya moyo. Tutashirikiana nao kwenye safari zetu mbalimbali ambapo wataalam wao watakwenda kutoa elimu na vipimo"
"Ushirikiano wa Yanga na Taasisi hii ya moyo utakuwa na manufaa makubwa kwa wamachama wa Yanga. Kila mwanachama wa Yanga ambaye ataenda kupata huduma atapata punguzo la 20%. Kwahiyo kwa wanachama ambayo hawajalipia ada zao ni muda sasa na kwa shabiki ambaye hajapata kadi yake ni muda sasa ili uweze kunufaika na huduma hizi," alisema