TFF yakanusha kubadili waamuzi wa mchezo wa watani wa jadi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
26 Apr 2018
TFF yakanusha kubadili waamuzi wa mchezo wa watani wa jadi
Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi ndani ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) Salum Umande Chama amesema waamuzi waliopangwa kuchezesha mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga hawajabadilishwa kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Chama amewataja waamuzi ambao watasimamia mchezo huo utakaochezwa Jumapili Aprili 29, 2018 kwenye uwanja wa taifa.

“Waamuzi tuliowapanga hawajabadilishwa ni walewale, mwamuzi wa kati ni Emanuel Mwandembwa (Arusha), line one Frank Komba (Dar), line two Mohamed Mkono (Tanga) na fourth official ni Hery Sasii”-Salum Umande Chama.

“Hawa ni waamuzi wa kimataifa ukizingatia kwamba Emanuel Mwandembwa amepata badge ya Fifa msimu huu kwa sasa yupo Burundi anachezesha mashindano ya U17 Burundi.”

“Mohamed Mkono pia amepata badge ya Fifa msimu huu na yeye yupo Burundi anachezesha mashindano ya Caf.”

“Frank Komba ni mwamuzi mzoefu kwa hiyo naamini watachezesha vizuri na mshindi atapatikana kwa njia halali.”

ShaffihDauda
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →