Meneja wa Yanga, Walter Harrison amefungiwa michezo mitatu na faini ya Sh 1 milioni na kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania akituhumiwa na kosa la kuwashurutisha waamuzi waliochezesha mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union kufanya maamuzi kwa mujibu wa wa maoni yake
Katika mchezo huo Walter alitumia kopyuta ndogo kuwaonesha marudio ya picha mjongeo (video) ya matukio mbalimbali ya mchezo huo kama ushahidi wa yale aliyokuwa akiyalalamikia
Kitendo hicho kimetafsiriwa na kamati kama kinachoweza kushawisi shari au vurugu uwanjani
Aidha klabu ya Yanga imepigwa ya jumla ya Tsh Milioni 12 kutokana na makosa yaliyojitokeza katika mechi zilizopita
Yanga imetozwa faini ya Sh 10 Milioni kwa kosa la kutumia mlango usio rasmi kuingia Uwanjani siku ya mchezo dhidi ya Simba kinyime na kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo
Yanga pia imetozwa faini ya Sh1 Milioni kwa kosa la kukataa kutumia chumba maalumu cha kubadilishia Nguo kwenye Uwan-ja wa Mkapa kinyume na kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo
Yanga imetozwa faini ya Sh 1Milioni kwa kosa la kuwakiliswa na kocha Mkuu pekee kwenye mkutano wa Wanahabari kueleke mchezo huo kinyume na natakwa ya kanuni ya 17:58 ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo inayotaka aambatane na nahodha ama mchezaji mwenye ushawishi Kikosini