Baada ya mapumziko ya takribani wiki tatu, Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) imerejea ambapo leo Jumanne, Yanga Princess itacheza mechi yake ya kwanza nyumbani msimu huu dhidi ya Mashujaa Queens
Mchezo huo utapigwa katika uwanja wa KMC Complex, saa 10 jioni
Huu ni mchezo ambao Yanga Princess itahitaji kushinda ili kuweka hai matumaini ya kuwania ubingwa msimu huu
Yanga Princess ililazimishwa sare katika mechi mbili zilizopita ugenini dhidi ya Bunda Queens na Alliance Girls
Hata hivyo Yanga Princess inasubiri maamuzi ya Kamati baada ya kuishitaki Alliance Girls kwa kuchezesha mchezaji ambaye hakuwa na sifa katika mchezo baina ya timu hizo
