Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema wako tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tabora United ambao utapigwa kesho Alhamisi katika uwanja wa Azam Complex
Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari, Gamondi alisema wanakwenda kuikabili Tabora United wakihitaji kushinda ili kwenda kwenye mapumziko ya FIFA wakiwa kileleni
Katika mchezo huo, Gamondi amesema atawakosa baadhi ya wachezaji kutokana na kadi tatu za njano na majeruhi lakini hana hofu kwa sababu ana kikosi kipana
"Tuko tayari kwa mchezo tuna changamoto ya kadi za njano na majeraha kwa baadhi ya wachezaji lakini tuko tayari"
"Yanga ni timu kubwa tuko kileleni mwa msimamo wa ligi lakini lazima tuheshimu wapinzani wetu"
"Tunafahamu aina ya mbinu ambazo timu hutumia wanapokuja kucheza nasi uwanja wa Azam Complex"
"Jambo la muhimu ni sisi kufungua mchezo na kutumia vyema nafasi tutakazotengeneza"
"Nimewasoma Tabora United, sasa wana kocha mpya na wameshinda mechi mbili zilizopita. Ni timu yenye wachezaji wengi wenye uzoefu, hili linaweza kutupa ugumu katika mchezo huo"
"Tulipoteza mchezo uliopita lakini matokeo hayo hayawezi kututoa katika malengo yetu. Wachezaji wangu walipata huzuni kwa kupoteza mchezo lakini mchezo huo umetupa funzo kuelekea mechi nyingine zote zinazofuata," alisema Gamondi
Gomondi amesisitiza ratiba imempa wakati mgumu katika maandalizi kwani wamekosa muda wa kuiandaa timu, wamecheza mechi 7 katika kipindi cha siku 20