Leo saa 12 jioni Yanga itakuwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuikabili Tabora United katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Unaweza kusema ni mtihani mwingine kwa safu ya ushambuliaji ya Yanga ambayo bado haijafanya kile kilichotarajiwa na Wananchi msimu huu
Washambuliaji Prince Dube, Kennedy Musonda, Jean Baleke na Clement Mzize bado wanakazi ya kufanya kwani takwimu zao hazivutii
Dube alianza vyema msimu akifunga mabao katika mechi za kirafiki, Ngao ya Jamii na ligi ya mabingwa hatua ya awali lakini bado ufanisi wake haujaonekana kwenye ligi
Baleke, Mzize na Musonda kila mmoja amefunga bao moja tu wakati ligi ikielekea kuhitimisha mechi za raundi ya 10

Idadi kubwa ya mabao ya Yanga yamefungwa na viungo washambuliaji Maxi Nzengeli akiwa kinara na mabao matatu
Wengine waliopachika mabao ni Pacome Zouzoua mwenye mabao mawili, beki Ibrahim Bacca (2), Clatous Chama (1) na Stephane Aziz Ki (1)
Yanga inahitaji kushinda dhidi ya Tabora United leo ili kuhakikisha inarejea kileleni katika msimamo wa ligi