Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina tayari ameanza rasmi kibarua cha kuinoa ZESCO United.
Kuanza kwake kazi ZESCO kunamaanisha Mzambia huyo tayari amemalizana na uongozi wa Yanga kwani mkataba wake ulikuwa ukimalizika mwishoni mwa msimu.
Katika barua yake ya kujiuzulu kocha huyo alitoa notisi ya miezi mitatu kama inavyotaka sheria na alikuwa tayari kulipa gharama ya muda uliobaki.
Hata hivyo Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema kocha huyo alikuwa na madai yake kwa klabu hivyo kufikia makubaliano ya kumalizana kistaarabu.
ZESCO imetinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa Barani Afrika.
Kabla ya kutua Yanga Lwandamina aliinoa ZESCO na kuiwezesha kutinga nusu fainali ya michuano hiyo mwaka 2016.
Yanga tayari imepata kocha kutoka Congo, Mwinyi Zahera ambaye pia ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya DR Congo.

ADVERTISE HERE