Beki wa kati wa Yanga Ibrahim Bacca ni miongoni mwa wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wanaoendelea na maandalizi kuelekea mechi za kuwania kufuzu michuano michuanao ya Afcon 2025 dhidi ya Ethiopia na Guinea
Licha ya kuendelea kukosekana katika kikosi cha Yanga akitumikia adhabu ya kadi nyekundu, Bacca yuko imara kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa
Yeye pamoja na Dickson Job ni wachezaji tegemeo katika safu ya ulinzi ya kikosi cha kocha Hemed Suleiman 'Morocco'
Job amemaliza adhabu ya kadi tatu za njano na hivyo atakuwa tayari kuitumikia Yanga katika mechi zitakazofuata kwenye ligi huku Bacca akitarajiwa kukosa mechi nyingine mbili
Nyota wengine wa Yanga ambao wako katika majukumu ya timu ya Taifa ni Clement Mzize na Mudathir Yahya