Yanga Princess leo imeshindwa kutamba mbele ya watani zao Simba Queens ikichapwa bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex
Kupoteza mechi ya Derby ni jambo moja, mbaya zaidi ni kuwa Yanga Princess imecheza mechi ya nne mfululizo pasipo kushinda
Imeambulia alama tatu kutoka sare tatu na leo kupoteza alama zote tatu katika mchezo ambao hawakutengeneza nafasi nyingi
Uongozi wa Yanga msiimu huu umefanya uwekezaji mkubwa kwa Yanga Princess lakini ni wazi uvumilivu bado unahitajika
Pengine pia maombi kwa timu hii yanahitaji ili angalau ianze kushinda kwani mambo yakiendelea hivi vita kubwa inaweza kuwa ni kupambana kubaki ligi kuu na sio kuwania ubingwa
ADVERTISE HERE