Kiungo wa Yanga Khalid Aucho ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa ya Uganda, ameiongoza timu hiyo kufuzu kwa fainali za Afcon 2025 zitakazofanyika mwakani nchini Morocco
Uganda wamefuzu pasipo kushuka uwanjani jana baada ya Sudan Kusini kuichapa Congo mabao 3-2
Vinara hao wa kundi K wamekusanya alama 10 kutoka mechi nne wakifuatiwa na Afrika Kusini iliyokusanya alama nane zote zikiwa zimefuzu
Aucho anaungana na Stephane Aziz Ki ambaye Burkina Faso ilikata tiketi mapema
Aziz Ki na mastaa kadhaa hawakuitwa katika kikosi cha Burkina Faso kwa ajili ya mechi mbili za kukamilisha ratiba. Pengine kwa sababu walishafuzu
ADVERTISE HERE