Mshambuliaji wa Yanga na timu ya Taifa ya Zambia Kennedy Musonda amekuwa na wakati mzuri katika michuano ya kuwania kufuzu Afcon 2025
Musonda ameisaidia Zambia kufuzu kwa michuano hiyo akipachika mabao matatu na kuwa miongoni mwa wachezaji waliofunga mabao mengi
Mshambuliaji wa Guinea, Serhou Guirassy anaongoza orodha hiyo akiwa amefunga mabao sita akifuatiwa na Brahim Diaz wa Morocco aliyepachika mabao manne
Musonda anafuatia na mabao yake matatu akifungana na Amine Gouiri (Algeria), Jean-Philippe Krasso (Ivory Coast), Sadio Mane (Senegal), Ryan Mendes (Cape Verde) na Trezeguet (Egypt)
Ni wazi Wananchi wanatamani kuona Musonda anarudi na kasi hiyo ya kutupia kwenye ligi kuu
Bila shaka kocha Sead Ramovic atakuwa akitabasamu akiangalia kazi nzuri inayofanywa na nyota wa Yanga ambao wako katika majukumu ya timu za Taifa