Gamondi ameacha rekodi za kibabe Jangwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2024
Gamondi ameacha rekodi za kibabe Jangwani

Miguel Gamondi alijiunga na Yanga Juni 24, 2023 akichukua nafasi ya Mtunisia Nasreddine Nabi aliyeipa mataji mawili ya Ligi Kuu, mawili ya Kombe la Shirikisho (ASFC), mawili ya Ngao ya Jamii na kuifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Tangu ateuliwe kukiongoza kikosi hicho, Gamondi amekiongoza katika jumla ya michezo 40 ya Ligi Kuu Bara kuanzia msimu wa 2023-2024, hadi huu wa sasa wa 2024-2025, ambapo kiujumla kati ya hiyo ameshinda 34, sare minne na kupoteza pia minne.

Katika michezo hiyo 40 ya msimu uliopita na huu wa sasa, safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho cha Gamondi imefunga jumla ya mabao 85 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 18, ambapo kiujumla kwa misimu miwili amekusanya pointi zake 104.

Gamondi amechukua mataji matatu na timu hiyo akianza na Ligi Kuu Bara msimu uliopita na kukifanya kikosi hicho kufikisha jumla ya mataji 30, tangu mwaka 1965, akachukua pia Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) na Ngao ya Jamii kwa msimu huu. Gamondi aliipeleka timu hiyo hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 25, kufuatia kufanya hivyo mara ya mwisho 1998.

Ushindi wa mabao 4-0, ilioupata Yanga dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria Februari 24, 2024, katika hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika, ulimfanya Gamondi kuandika rekodi mpya ya kuivusha robo fainali kwa mara ya kwanza kwenye historia yao.

Gamondi aliandika rekodi nyingine mpya ya kibabe kwa kuifanya Yanga iwe ya kwanza nchini kushinda mabao mengi zaidi kwa timu za Kaskazini.

Ushindi huo wa mabao 4-0, dhidi ya CR Belouizdad uliifanya kuivuka rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Simba katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018-2019 ambapo ilikuwa ya kwanza nchini kuifunga JS Saoura ya Algeria kichapo cha mabao 3-0.

Moja ya jambo kubwa litakalokumbukwa kwa Gamondi ni kuiwezesha timu hiyo kushinda kwa mabao 5-1, dhidi ya Simba Novemba 5, 2023, yaliyofungwa na mastaa, Kennedy Musonda, Stephane Aziz KI na Pacome Zouzoua huku Maxi Nzengeli akifunga mawili.

Simba ilikuwa haijawahi kufungwa na Yanga idadi kama hiyo kubwa ya mabao tangu ilipolazwa 5-0 mwaka 1968, kipigo ambacho Simba ilikilipa kwa kishindo mwaka 1977 kwa kuifumua Yanga 6-0 kisha kupigilia msumari mwingine wa mabao 5-0 mwaka 2012.

Kichapo hicho kilimfukuzisha kazi Kocha Mbrazili, Roberto Oliveira β€˜Robertinho’, ambaye alikuwa na rekodi nzuri mbele ya Yanga akiifunga mara tatu kwenye mechi tofauti ikiwemo ya Ligi Kuu Bara na Ngao ya Jamii, japo mambo yote yalibadilika

Lakini pia Gamondi ameondoka akiwa ameshinda mechi zote dhidi ya Simba katika ligi kuu. Mchezo pekee aliopoteza ni Ngao ya Jamii msiimu uliopita tena kupitia mikwaju ya penati baada ya matokeo ya suluhu ya bila kufungana

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Goals; CFFA 0-4 Yanga (FT)
Goals; CFFA 0-4 Yanga (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL R1
FT : CFFA 0-4 Yanga, CAFCL R1
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : CFFA vs Yanga, CAFCL R1
Kikosi : CFFA vs Yanga, CAFCL R1
4h ago
READ MORE β†’
Matchday; CFFA vs Yanga, CAFCL R1
Matchday; CFFA vs Yanga, CAFCL R1
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 17 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 17 2026
11h ago
READ MORE β†’
Diarra hatihati kuikoa CFFA
Diarra hatihati kuikoa CFFA
23h ago
READ MORE β†’
Yanga kusaka rekodi ya kufuzu makundi kwa msimu wa nne mfululizo
Yanga kusaka rekodi ya kufuzu makundi kwa msimu wa nne mfululizo
1d ago
READ MORE β†’
Manqoba aweka mkazo, hawatawadharau CFFA
Manqoba aweka mkazo, hawatawadharau CFFA
1d ago
READ MORE β†’
CFFA vs Yanga; Tiketi zinaelekea ukingoni, umekata yako?
CFFA vs Yanga; Tiketi zinaelekea ukingoni, umekata yako?
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 16 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 16 2026
1d ago
READ MORE β†’