Klabu ya Yanga imeirejesha nafasi ya Mkurugenzi wa ufundi ambapo leo wamemtangaza AbduHamid Moallin kushika nafasi hiyo
Mdachi Hans van Pluijm alishika nafasi hiyo mara ya mwisho mwaka 2016 Yanga ilipomuajiri kocha George Lwandamina
Kabla ya kujiunga na Yanga, Moallin alikuwa Kocha Mkuu wa KMC ambayo aliachana nayo wiki iliyopita
Kwa cheo chake, Moallin sasa ndiye msimamizi mkuu wa dira na masuala yote ya kiufundi ndani ya Yanga
Huyu ndiye kiunganishi kati ya uongozi wa Yanga na benchi la ufundi
Karibu Jangwani Moallin...!
ADVERTISE HERE