Nevemba 26 ni siku maalum kwa mashabiki wa Yanga kwani ndio siku ambayo mchezo wa ufunguzi hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika utapigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ni mchezo wa kisasi dhidi ya Al Hilal ya Sudan. Ni DUBE DAY, siku ya kufungua milango yote iliyofungwa
Mauzo ya tiketi yameanza mapema hivyo kwa Mwananchi ambaye huna tiketi, unapaswa kuhakikisha umepata yako mapema
Yanga inakwenda katika mchezo huu ikiwa na dhamira moja tu, kuibuka na ushindi ili kuanza vyema hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa msimu huu
Katika misimu miwili iliyopita, Yanga haikuanza vyema hatua ya makundi ikipoteza mechi zote za ufunguzi ambazo zilipigwa ugenini
Lakini wakati huu safari inaanzia nyumbani, ni muhimu safari hiyo ikaanza mbele ya mashabiki 60,000 pale uwanja wa Benjamin Mkapa