Ibenge amuhofia Ramovic

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Nov 2024
Ibenge amuhofia Ramovic

Mabadiliko katika benchi la ufundi la Yanga, yameonekana 'kumtisha', Kocha Mkuu wa Al Hilal Omdurman ya Sudan, Florent Ibenge, ambaye amesema yeye alijiandaa kupambana na aliyekuwa Kocha Mkuu, Miguel Gamondi na si Mjerumani, Sead Ramovic

Yanga ilitangaza kuchana na Gamondi wiki iliyopita na Ramovic kutoka TS Galaxy ya Afrika Kusini alikabidhiwa mikoba ya kuwaongoza mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara

Akizungumza jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa hatua ya makundi wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Ibenge, alisema maandalizi waliyokuwa wameyafanya awali ni kwa ajili ya kukabiliana na mfumo unaoongozwa na Gamondi

Ibenge alisema kwa nyakati mbalimbali alikuwa 'ameshamsoma' na kujua mbinu za Gamondi na kukiandaa kikosi chake kukabiliana na ushindani huo, lakini ujio na Ramovic, umemchanganya

"Tulishamjua aina yake ya uchezaji na mifumo ya Gamondi, tulifanyia kazi namna timu yake inavyocheza, huyu mpya kwetu itakuwa ni mgumu sana, hatujui lolote, hatujui atakuja na mbinu gani. Tunatakiwa kuwa makini sana," alisema Ibenge.

Mkongomani huyo alisema kundi lao lenye timu za Yanga, Al Hilal, MC Alger ya Algeria na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DR Congo), ni gumu na kila timu ina uwezo wa kuifunga timu nyingine na kutinga hatua ya robo fainali

"Kila timu inataka kwenda robo fainali na kundi letu (Kundi A), timu yeyote inaweza kumfunga mpinzani, zina uzani na ubora unaolingana, hivyo tunatakiwa tupate pointi nyingi kwa kadri inavyowezekana," alisema Ibenge

Aliongeza kwa sababu hiyo aliamua kuwasili nchini mapema kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya mchezo huo ambayo ni pamoja na kuzoea hali ya hewa ya Dar es Salaam ambalo kwa sasa joto

Ni wazi Yanga inaweza kunufaika na mabadiliko ya benchi la ufundi kwani haitakuwa rahisi kwa Ibenge kutabiri Yanga itaingiaje katika mchezo huo na wakati huohuo Yanga inamfahamu vyema Ibenge na aina ya mbinu anazotumia katika mechi zake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
11h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
15h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
16h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
16h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’