Aziz Ki yuko 'full charge' kuwakabili Al Hilal

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Nov 2024
Aziz Ki yuko 'full charge' kuwakabili Al Hilal

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki amepata muda mzuri wa 'ku-recover' baada ya kutumika mfululizo na pengine mashabiki wa Yanga watarajie kumuona akirejea kivingine Novemba 26 katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal

Ukizungumzia wachezaji waliotumika zaidi na aliyekuwa kocha wa Yanga Miguel Gamondi, Aziz Ki ni mmoja wa wachezaji hao, nyota huyo pia alikabiliwa na majukumu ya timu ya Taifa ya Burkina Faso

Aziz Ki hakujumuishwa katika kikosi cha Burkina Faso kilichohitimisha mechi mbili za kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2025, Kocha wa kikosi hicho, Brama Traore alitaja sababu kwa nini hakumuita Aziz Ki

"Maamuzi yangu ya kumuacha Azizi Ki yana sababu mbili. Kwanza ni kutoa nafasi kwa wachezaji wengine ambao walikuwa hawaitwi timu ya Taifa baada ya kikosi chetu kufuzu kwenda Afcon," amesema.

"Sababu ya pili ni kutokana na kumpa muda wa kupumzika kwa kuwa alitumia nguvu kubwa msimu uliopita na pia namuona kama ana uchovu uliotokana na majukumu ya klabu yeke," alisema Traore katika mahojiano aliyofanya punde baada ya kutangaza kikosi chake mwanzoni mwa mwezi huu

Kwa kutojumuishwa timu ya Taifa, Aziz Ki amepata muda wa kupumzika pamoja na kufanya mazoezi na wachezaji wenzake waliokuwa wamebaki Avic Town

Licha ya mabadiliko ya benchi la ufundi, Aziz Ki bado anaonekana ni mchezaji muhimu katika kikosi cha kocha Sead Ramovic na bila shaka ataendelea kuwa mchezaji tegemeo katika kikosi cha Mjerumani huyo kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, Gamondi

Matarajio ya Wananchi ni kumshuhudia Aziz Ki akirejea katika kiwango bora kilichompa tuzo za mchezaji bora, mfungaji bora na kiungo bora msimu uliopita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
6h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’