Ni Gusa achia twende kwao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Nov 2024
Ni Gusa achia twende kwao

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametamba kuwa Jumanne katika mchezo dhidi ya Al Hilal, Yanga inakwenda kutambulisha mfumo mpya wa soka lake chini ya Kocha Sead Ramovic

Kamwe amesema mfumo huo wameupachika jina la 'GUSA ACHIA TWENDE KWAO..' kwa maana ndio aina ya soka ambalo Ramovic amelitambulisha viunga vya Avic Town, hakuna mchezaji anaruhusiwa na mpira wa dakika nyingi...!

"Jumanne ni siku ambayo Tanzania yote itatulia na kuufatilia mchezo wetu dhidi ya Al Hilal. Kocha wetu 'German Machine' Ramovic metambulisha Soka linaloitwa 'GUSA ACHIA TWENDE KWAO'

"Baada ya kutazama hili soka mazoezini nikaona kabisa Wananchi tunakwenda kupata Raha siku ya Jumanne, Niwaombe msiwe watu wa kuikosa furaha hii, tukate tiketi muda huu tukutane Benjamin Mkapa kufurahi pamoja," alisema Kamwe

Akizungumza na Wananchi waliojitokeza kwa wingi Karume sokoni mapema leo, Kamwe amewataka kila mmoja kununua tiketi yake ili kuhakikisha Jumanne hata nafasi ya kutema mate inakosekana pale uwanja wa Benjamin Mkapa

"Tunafahamu kuwa mchezo wetu dhidi ya Al Hilal utakuwa mgumu lakini kwa umoja wetu, kwa wingi wetu, kwa hamasa tutakayowapa wachezaji wetu, mchezo huu utakuwa Mwepesi na tutashinda"

"Wachezaji wetu wapo Tayari, benchi la ufundi lipo tayari na viongozi wetu wapo tayari, kazi iliyobaki ni kwetu sisi Wananchi, Jukumu letu ni kuwasapoti wachezaji wetu, basi tukate Tiketi kwa wingi na twende kwa wingi kuishangilia Yanga yetu"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’