Kikosi cha Yanga leo asubuhi kimefanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuelekea mchezo wa kwanza hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal ambao utapigwa kesho Jumanne, Novemba 26 katika uwanja huo
Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic aliongoza 'session' hiyo ya mwisho, kazi iliyobaki ni kwa vijana wake ni kukamilisha kile walichojifunza na kuwapa furaha mashabiki wao hapo kesho
Wapinzani wao Al Hilal ambao wako jijini Dar es salaam tangu wiki iliyopita, jioni watafanya mazoezi katika dimba la Mkapa ikiwa ni kwa mujibu wa kanuni
Bado tiketi zinapatikana, mashabiki wameaswa kuendelea kununua tiketi ili kuhakikisha uwanja wa Mkapa unakuwa 'full house' hapo kesho
Mpaka sasa tiketi zimebaki chache katika madaraja ya VIP B, VIP C na Mzunguuko