FT : Yanga 0-2 Al Hilal

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Nov 2024
FT : Yanga 0-2 Al Hilal

Yanga imeshindwa kutamba uwanja wa Benjamin Mkapa ikikubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Al Hilal katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika

Bado makosa katika safu ya ulinzi yameendelea kuigharimu Yanga ikiruhusu mabao kupitia mashambulizi ya kushitukiza

Yanga ilianza mchezo huo taratibu na kuongeza kasi kipindi cha pili lakini Florent Ibenge alitumia vyema silaha ya mashambulizi ya kushitukiza akitumia mawinga wake wenye kasi

Kocha Saed Ramovic ana kazi ya kuboresha eneo la umaliziaji kwani bado inakuwa ngumu kufunga dhidi ya timu zinazopaki basi

Yanga inahitaji kushinda angalau mechi inayofuata ili kurudisha ari ya ushindi katika timu

Ni nyakati ambazo kila timu bora hupita, muhimu ni kwa kiasi gani benchi la ufundi na wachezaji wenyewe watapambana katika uwanja wa mazoezi ili kurejea kwenye ubora

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
7h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
15h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
19h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’