Ukiangalia mechi tatu ambazo Yanga imepoteza katika michuano yote, ni rahisi kubaini aina ya makosa yaliyopelekea kuadhibiwa yanafanana
Al Hilal leo wamefanya kile kilichofanywa na Tabora United katika mchezo uliopita ambao Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-1
Ni kama kocha wa Al Hilal Florent Ibenge alinasa faili ambalo kocha wa Tabora United alilitumia kumuadhibu Miguel Gamondi katika mchezo uliopita
Kwa bahati mbaya Sead Ramovic akarejea na mfumo uleule ambao ulipelekea kupoteza mchezo uliopita
Yanga inaposhambulia inakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kufungwa kupitia mashambulizi ya kushitukiza
Kuna udhaifu katika eneo la kiungo, pengine kukosekana kwa Khalid Aucho leo kumechangia kwa kuwa Mudathir Yahya na Duke Abuya kwa asili sio viungo wakabaji hivyo hawakai katika maeneo yao
Yanga pia inashindwa kufungua timu ambazo zinapaki basi, timu inatengeneza mashambulizi taratibu jambo ambalo linawapa wapinzani muda wa kujipanga kuzuia
Kuna madhaifu ya wazi yanaonekana, timu inacheza taratibu sana, ile 'intensity' ya msimu uliopita haionekani, hapa kocha wa viungo ana kazi ya kufanya pia
Kupoteza mechi tatu mfululizo sio matokeo ya yanayoweza kupokelewa kirahisi, ni wazi benchi la ufundi wanapaswa kufanya kazi haraka katika uwanja wa mazoezi kuirejesha timu katika ubora