Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesema kupoteza mchezo dhidi ya Al Hilal imechangiwa na wachezaji wake kutokuwa katika kiwango bora cha utimamu wa mwili
Ramovic amesema ili timu iweze kushindana katika michuano mikubwa ni lazima 'fitness' ya wachezaji iwe juu
Amesema wanarudi katika uwanja wa mazoezi kufanyia kazi mapungufu hayo ili kuhakikisha wanarejea wakiwa imara zaidi
"Haukuwa mwanzo mzuri kwangu binafsi na hata timu nzima katika michuano hii lakini tunapaswa kuwa wawazi, nitazungumzia maeneo ambayo tunahitaji kuyaboresha"
"Miongoni mwa maeneo yaliyotuangusha ni utimamu wa mwili wa wachezaji wangu. 'fitness' ya wachezaji iko chini sana. Kama unataka kufanya vizuri katika michuano ya ligi ya mabingwa 'fitness' ya wachezaji lazima iwe juu"
"Tumeshindwa kucheza kikamilifu kwa dakika 90 kwa sababu hiyo ya fitness ya wachezaji kuwa chini. Tulianza mchezo vizuri, tulipata nafasi kadhaa za kufunga lakini hatukuzitumia"
"Kipindi cha pili tulikuwa na nafasi bora zaidi mbele ya lango la Al Hilal, Mipira ya kichwa ya Aziz Ki na Kennedy Musonda, kama tungezitumia pengine tungebadili taswira ya mchezo. "
"Tumekubali matokeo, ni mechi moja tumepoteza hivyo bado ni mapema. Tuna muda wa kufanyia kazi changamoto zetu na kuboresha ili tufanye vizuri katika mechi zinazofuata. Naamini tutarejeea tukiwa imara zaidi" alisema Ramovic