Beki wa Yanga Dickson Job amewaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo kufuatia mwenendo mbaya wa timu yao
Yanga ilipoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika jana kwa kufungwa na Al Hilal ya Sudan mabao 2-0, na kuifanya timu hiyo kupoteza michezo mitatu mfululizo
Awali Yanga ilipoteza michezo miwili ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC (1-0) na Tabora United (3-1)
Job ametumia ukurasa wake wa Instagram kufikisha ujumbe kwa mashabiki wa Yanga akiandika:
"Wananchi, Poleni sana kwa kipindi kigumu tunachopitia, Nafahamu Maumivu haya yanachagizwa na ukweli kwamba mnaipenda kwa dhati timu yenu na mnatuamini sana wachezaji wenu"
"Lakini msisahau Wananchi, hakuna wakati sisi tunakua imara kama pale tunapopitia magumu. Nyie mnakumbuka nyakati nyingi tulizozomewa na watu wote tulisimama tena kwa matumaini na kuishangaza dunia ya wapenda soka"
"Wananchi, tuchane kalenda yenye kumbukumbu zote mbaya na tuanze upya kwa kasi na tamaa ya kuendelea kuwafanya mjivunie kuwa mashabiki wa klabu bora zaidi kwenye taifa letu," aliandika Job