Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic keshokutwa Jumamosi atakiongoza kikosi chake katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu ambapo Yanga itakuwa ugenini dhidi ya Namungo Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Majaliwa, Ruangwa
Ramovic hakuanza vyema majukumu yake juzi akiwashuhudia vijana wake wakipoteza mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya Al Hilal
Hata hivyo kocha huyo raia wa Ujerumani alikuwa na takribani siku nane tu tangu alipokabidhiwa mikoba ya kuinoa Yanga baada ya mabingwa hao wa Tanzania Bara kumfuta kazi Miguel Gamondi
Jumamosi ataiongoza Yanga katika mchezo wa pili, lakini utakuwa wa kwanza kwenye ligi, atahitaji kushinda mchezo huu ili kurejesha ari ya ushindi ya kikosi chake
Baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo, Yanga inazihitaji sana alama tatu za mchezo dhidi ya Namungo Fc kabla ya kusafiri Algeria kuifuata MC Alger ambayo watachuana nayo katika mchezo wa pili hatua ya makundi CAF CL, Disemba 07
Lakini pia Yanga imezidiwa alama nne na watani zao Simba, matokeo tofauti na ushindi yatafanya gap la pointi kuongezeka lakini ushindi utazitofautisha timu hizo kwa alama 1
Mara nyingi mechi dhidi ya Namungo Fc sio nyepesi, hivyo hii ni kama mechi ya fainali kwa Yanga, hakuna nafasi ya kupoteza mechi zaidi...Β