Yanga iko tayari kuikabili Namungo Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Nov 2024
Yanga iko tayari kuikabili Namungo Fc

Kikosi cha Yanga jioni ya leo Ijumaa Novemba 29 kimekamilisha maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Majaliwa

Ari na morali ya wachezaji wa Yanga inaonekana kuwa juu, ni wazi dhamira yao ni kuona kesho wanamaliza wimbi la kupoteza mechi mfululizo

Mazoezi ya mwisho yamefanyika katika uwanja wa Majaliwa ambao mchezo huo utapigwa saa 12:30 jioni

Itakuwa mechi ngumu lakini hakuna namna, ni mechi ambayo Yanga haihitaji matokeo mengine zaidi ya ushindi

Yanga inatarajiwa kupata sapoti kubwa ya mashabiki wake kutoka maeneo mbalimbali ambao wamesafiri kwenda Ruangwa

Takribani mabasi 10 yameondoka jijini Dar es salaam kuelekea Ruangwa, Lindi yakibeba Wanachama kutoka matawi mbalimbali

Katika kuonyesha kuiunga mkono timu yao katika hali zote, Wananchi wataujaza uwanja wa Majaliwa ili kuwaongezea hamasa wachezaji wao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kwa Toure hapa Yanga imepata mshambuliaji
Kwa Toure hapa Yanga imepata mshambuliaji
2h ago
READ MORE β†’
Kangwanda ana kazi ya kufanya Yanga
Kangwanda ana kazi ya kufanya Yanga
4h ago
READ MORE β†’
Kocha tayari amewasili tutamtambulisha wakati wowote - Kamwe
Kocha tayari amewasili tutamtambulisha wakati wowote - Kamwe
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 02 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 02 2026
6h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 4-0 Kagera Sugar, NBC PL (FT)
Highlights : Yanga 4-0 Kagera Sugar, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 4-0 Kagera Sugar, NC PL, Nov 1
FT : Yanga 4-0 Kagera Sugar, NC PL, Nov 1
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Kagera Sugar, NBC PL, Nov 1
Kikosi : Yanga vs Kagera Sugar, NBC PL, Nov 1
19h ago
READ MORE β†’
Matchday : Yanga vs Kagera Sugar, NBC PL, Nov 1
Matchday : Yanga vs Kagera Sugar, NBC PL, Nov 1
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 01 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 01 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mzize arejeshwa kikosi cha Stars
Mzize arejeshwa kikosi cha Stars
1d ago
READ MORE β†’