Ramovic afurahia ushindi wa kwanza Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Dec 2024
Ramovic afurahia ushindi wa kwanza Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amewapongeza vijana wake kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Majaliwa jana

Akizungumza baada ya mchezo huo, Ramovic alisema ni alama tatu muhimu kwao hasa baada ya kupoteza mechi zilizopita

Ramovic aliwashukuru mashabiki waliojitokeza kwa wingi kuiunga mkono Yanga katika mchezo huo ambao walihitaji sana sapoti yao

Licha ya ushindi huo, Ramovic alisema bado kuna kazi ya kufanya katika uwanja wa mazoezi ili kuimarisha zaidi

"Bado tuna safari ndefu msimu huu lakini nadhani matokeo haya ni muhimu kwetu kwa wakati huu. Nawapongeza wapinzani wetu, haikuwa rahisi kwani walikuwa wazuri katika mbinu zao kwenye kuzuia"

"Ni alama tatu kwetu lakini bado tunahitaji kujiimarisha zaidi. Bado kuna maeneo mengi tunahitaji kuboresha likiwemo eneo la 'fitness'. Najua sio rahisi lakini tutaendelea kuimarika taratibu"

"Sasa tunakwenda kujiandaa kwa ajili ya mchezo unaofuata (CAF CL dhidi ya MC Alger), ni mechi muhimu sana kwetu lakini naamini baada ya kupata ushindi leo, tutakwenda katika mchezo huu tukiwa na fikra tofauti," alisema Ramovic

Jana Yanga ilionyesha utofauti mkubwa, timu ilishambulia kwa kasi na walihakikisha wapinzani wao hawapati nafasi ya kumiliki mpira

Pale walipopoteza mpira, 'wali-press' haraka kuurejesha katika himaya yao. Hii ndio aina ya soka ambalo Ramovic anataka kuwaona vijana wake wakicheza

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ratiba ya mwisho wa mwaka usipime
Ratiba ya mwisho wa mwaka usipime
1h ago
READ MORE β†’
Adnan Behlulovic humwambii kitu kwa Yanga
Adnan Behlulovic humwambii kitu kwa Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kazini kwa Kibwana bado kuna kazi
Kazini kwa Kibwana bado kuna kazi
17h ago
READ MORE β†’
Shalulile atabiriwa makubwa msimu huu
Shalulile atabiriwa makubwa msimu huu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga kurudi New Amaan Complex makundi CAFCL?
Yanga kurudi New Amaan Complex makundi CAFCL?
1d ago
READ MORE β†’
Nyota tisa wa Yanga kwenye majukumu ya timu za Taifa
Nyota tisa wa Yanga kwenye majukumu ya timu za Taifa
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
1d ago
READ MORE β†’
Pacome aongeza matumaini ya kurejea mapema
Pacome aongeza matumaini ya kurejea mapema
1d ago
READ MORE β†’
Kwa Toure hapa Yanga imepata mshambuliaji
Kwa Toure hapa Yanga imepata mshambuliaji
2d ago
READ MORE β†’