Leo wakati miamba ya soka nchini Simba na Yanga ikiumana kwenye uwanja wa Taifa, nchini Burundi timu ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys ilikuwa ikichuana na Somalia kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya CECAFA.
Serengeti Boys imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 hivyo kutwaa taji la michuano hiyo inayohusisha timu za Africa Mashariki na Kati.
Katika michuano hiyo Uganda imemaliza ikiwa nafasi ya tatu na Kenya nafasi ya nne.
Hongera kwa vijana wa Tanzania kutwaa taji hilo. Kufanya vizuri kwa timu za vijana za Tanzania ni dalili nzuri na huenda wachezaji hao kama watatunzwa vizuri watakuja kuimarisha kikosi cha timu ya Tanzania ya wakubwa

ADVERTISE HERE