Kipigo cha pili mfululizo katika michuano ya ligi ya mabingwa kimewashtua mashabiki wa Yanga ambao sasa wanaiona hatari ya timu yao kutosonga mbele hatua ya robo fainali kama haitafanya vizuri katika mechi nne zilizobaki
Katika msimu ambao Yanga iliweka malengo makubwa ya kuvuka hatua ya robo fainali, hilo litawezekana tu kama kocha Sead Ramovic na vijana wake watachanga vyema karata katika mechi nne zilizosalia
Makosa katika safu ya ulinzi yameendelea kuigharimu Yanga kwa kuruhusu mabao katika nyakati ambazo haionekani kuwa ni hatari
Yanga ilicheza kwa nidhamu kubwa kwa dakika zote 45 za kipindi cha kwanza jana na kupeleka mchezo dhidi ya MC Alger kwenda mapumziko matokeo yakiwa sare ya 0-0 lakini mambo hayakwenda vyema katika kipindi cha pili
Mchezo unaofuata ni ugenini dhidi ya TP Mazembe ambao watacheza nao mechi mbili ugenini na nyumbani
Mechi hizo zitaamua hatma ya Yanga na malengo ya kutinga robo fainali. Mazembe walilazimishwa suluhu ya bila kufungana katika mechi yao ya kwanza nyumbani dhidi ya MC Alger
Leo wanacheza dhidi ya Al Hilal katiika mchezo ambao pengine Wananchi watatamani kuona unamalizika kwa sare au hata TP Mazembe kushinda ili kundi liendelee kuwa wazi
MC Alger wako kileleni kundi A wakiwa na alama 4 wakati Al Hilal wakiwa na alama 3 katika nafasi ya pili na TP Mazembe ikishika nafasi ya tatu na alama 1
Wananchi bado hawana alama yoyote wakiendelea kuburuza mkia katika kundi hilo